Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Huku mabadiliko makubwa kwenye mamlaka ya afya ya jamii (SHA) yakizidi kushuhudiwa kimfumo, wananchi wametakiwa kuzidi kujisajili ili kuweza kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali jimboni Marsabit.
Meneja wa bima ya (SHIF) eneo pana la Saku, North Horr na Laisamis, Mutuma Kaaria amewataka wananchi kuzidi kujiandikisha wao na familia zao ili kufanikisha na kurahisisha upokeaji wa matibabu.
Kulingana na Mutuma ni kuwa hospitali zote za serikali kuanzia kiwango cha level 1 na 3 zinatoa matibabu kwa wananchi bila usumbufu wowote.
Anasema hospitali za level 4 na 5 zinapokea wagonjwa waliopendekezewa kusaka matibabu Zaidi na hivyo huduma ya SHIF itasaidia kusimamia malipo hayo.
Hospitali saba za kibinafsi na mbili za kidini anasema zimetia kandarasi na serikali ili kutoa huduma hizo chini ya mpango wa SHIF