HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
NA NAIMA MOHAMMED
Wito umetolewa kwa wananchi katika kaunti ya Marsabit kudumisha usafi ili kujizuia dhidi ya maradhi yanayotokana na uchafu.
Kwa mujibu wa afisa anayesimamia maswala ya usafi katika kaunti ya Marsabit Chris Mabonga ni kuwa baadhi ya magonjwa ambayo yanaripotiwa hapa jimboni Marsabit yanaweza epukika iwapo wananchi watadumisha usafi wa kiwango cha juu.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Mabonga amesema kuwa kero la ukosefu wa maji katika maeneo mengi hapa jimboni linasabisha uwepo wa magonjwa huku akiirai serekali ya kaunti kuhakikisha kwamba inasambaza maji hadi vijijini ili kuwaepusha wananchi na baadhi ya maradhi.
Aidha Mabonga ametoa wito kuhakikisha kwamba wananchi wana vyoo vijijini ili kuzuia pia baadhi ya magonjwa yanayotokana na ukosefu wa choo.