HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na JB Nateleng,
Wito umetolewa kwa wahudumu wa afya katika kaunti ya Marsabit kufanya mazungumzo na serekali ya kaunti ili kumaliza mgomo ambao umeathiri sekta ya afya hapa jimboni.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Chifu wa lokesheni ya Kalacha Sabdio Wario amesema kuwa itakuwa ni afueni iwapo serekali itashughulikia malalamishi ya wahudumu wa afya na pia kushirikiana nao katika kutoa suluhu la kudumu ambalo litasaidia katika kuboresha sekta ya afya ambayo ndio uti wa mgongo wa jamii.
Sabdio ameelezea kuwa mgomo huu huenda ukasababisha madhara mengi ambayo yanafaa kuangazia mapema kwa kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya wanapata haki yao ili kuwapa motisha na pia kuhakikisha kwamba wanawapa wananchi huduma Bora.
Kadhalika Sabdio ameelezea kuwa kufikia sasa wafugaji wengi katika eneo la Kalacha wameanza kutumia dawa za kienyeji kutokana na kushindwa kumudu gharama za juu za dawa kutoka kwa kliniki za kibinafsi.