WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wito umetolewa kwa jamii ya Marsabit kutowaficha watoto waliona ulemavu na badala yake kuhakikisha kwamba wanapata haki zao za kimsingi.
Kwa mujibu wa meneja wa kituo cha huduma Center mjini Marsabit Geoffrey Ochieng ni kuwa watoto waliona ulemavu wanafaa kupewa haki sawa za masomo na za kimaisha kama wenzao wasio na ulemavu.
Akizunguma baada ya wafanyikazi wa kituo hicho kutembelea watoto walio na ulemavu wa kusikia katika shule ya msingi ya SKM, Ochieng ameweka wazi kuwa iwapo watoto hao watapewa nafasi kama watoto wengine basi wanaweza kufanya majukumu kama watu wengine.
Ameitaka jamii pia kuwaangazia watoto wanaoishi na ulemavu sawa na wanavyowaangazia na kujukumisha watoto wengine.
IAidha Ochieng ametaja kwamba wanapania kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi kama njia ya kusherekea wiki ya huduma kwa umaa wiki hii.