IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
NA LELO WAKO NA JOB KOROWA
Mratibu wa maswala ya watoto katika parokia ya Marsabit Sisiter Agatha Gatimu ameeleza kuwa kanisa lina mpango wa kuwafunza watoto kanisani na kuwashughulisha katika mashindano tofauti haswa wakati huu wa likizo ya muhula wa pili.
Akizungumza na idhaa hii Sisiter Agatha ameeleza kuwa zoezi hilo linalenga kuwasaidia watoto ambao wako likizoni kutumia muda wao vyema ili kuepukana na maadili potovu.
Aidha Sister Agatha amewahimiza Watoto kuwa waangalifu na watiifu kwa wazazi huku akiwarai kuepukana na marafiki wapotovu ili kulinda maadili yao.
Ameto onyo dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa watoto kwani yanaadhiri afya yao na akili zao.
kadhalika amewahimiza wazazi kuwafuatilia wanachokifanya watoto wao kwenye mitandao huku akiwataka kuwa mifano miema kwao ili watoto wawe na watu wa kuiga katika jamii.