HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Watu saba wameaga dunia katika eneo la Elle-Dimtu baada ya lori walilokuwa wakisafiria kushambuliwa na wahalifu saa tano usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na DCC wa Marsabit Central David Saruni aliyezungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya kamishina wa kaunti Marsabit ni kuwa lori hilo lilishambuliwa na watu waliokuwa wamevalia sare za kijeshi kutoka taifa jirani la Ethiopia.
Saruni ametaja kwamba mmoja kati ya watu Saba ambao wameaga dunia hajatambuliwa japo wengine sita wameweza kutambuliwa.
Hata hivyo Saruni ameweka wazi kuwa watu wawili wanauguza majeraha huku mmoja akiwa katika hali mahututi.
Vilevile msichana mmoja aliepuka shambulizi hilo la usiku wa kuamkia leo.
Kadhalika Saruni ameweka wazi kuwa shambulizi hilo sio la mzozo wa kikabila bali ni wahalifu kutoka taifa jirani la Ethiopia huku akiwata wananchi kutoeneza uvumi ambao unaweza zidisha taharuki.
Amewataka wananchi kutoa taarifa muhimu kwa polisi ili kufanikisha uchunguzi.