WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wakaazi jimboni Marsabit na ambao hunufaika na msaada wa fedha kutoka kwa mpango wa HUNGER SAFETY NET wanatarajiwa kupokea fedha hizo kuanzia tarehe 3 mwezi ujao wa Novemba.
Haya ni kulingana na mkurugenzi wa mamlaka ya kukabiliana na ukame NDMA jimboni Marsabit Guyo Golicha ambaye amezungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee.
Guyo ameeleza kuwa mamlaka ya NDMA imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kifedha na hivyo kusababisha kuchelewa kwa fedha hizo.
Amesema kuwa watu wasiojiweza katika jamii na ambao wanaishi katika umaskini wa kiwango cha juu ndio hulengwa zaidi na mpango huo ili kuwahakikishia usalama wao wa chakula
Aidha Guyo ameweka wazi kuwa sio kila boma hunufaika licha ya kuwa wamesajiliwa chini ya mpango wa Hunger Safety Net.
Kulingana naye ni boma 21,000 kati ya boma 90,000 zilizosajiliwa jimboni amabazo hunufaika na fedha hizo.