Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Wakaazi wa Marsabit wahimizwa kupanda miti na pia mimea itakayokua kwa muda mfupi kama moja wapo ya njia kupambana na janga la njaa.
Akizungumza na shajara hii kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema kuwa jamii nyingi za Marsabit hawakumbatii kilimo kama njia moja ya kuondoa dhiki ya njaa katika eneo hili.
Vile vile kamishna Kamau amehimiza wakaazi pia kupanda miti haswa miti ya matunda ili kukabiliana na matatizo ya tabianchi katika eneo hili.
Wakati uo huo kwenye suala la umeme mashinani rural electrification iliyoziduliwa miezi michache na rais Wiliam Ruto kamishna Kamau amesema kuwa shule na hospitali ni maeneo ambayo yanalengwa.
Aidha amesema kuwa stima hizo za mashinani ni ya gharama nafuu itakayonufaisha wakaazi wa eneo hili.