Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Samwel Kosgei,
Wakaazi wa eneo la Demo wadi ya Turbi – Bubisa eneobunge la North Horr wameonesha masikitiko yao kufuatia madai ya kuharibiwa kwa barabara kutoka Demo kuelekea Bubisa na mwanakandarasi anayekarabati barabara hiyo.
Wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na Golo Galgalo wamesema kuwa kuchimbwa upya kwa barabara hiyo kumezidisha mahangaiko yao kwani imeharibika kiasi cha kutopitika hata kwa pikipiki.
Galgalo anasema imekuwa vigumu kufikiwa na chakula kutokana na barabara hiyo kutopitika kama ilivyokuwa hapo awali.
Aidha amesema iwapo mtu atahitaji matibabu ya dharura basi itakuwa vigumu kupata msaada wa haraka.
Sasa anamtaka mwanakandarasi aliyejukumishwa kurekebisha barabara hiyo kumaliza kwa kasi kwani wanapitia mahangaiko.