HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na JB Nateleng & Naima Abdullahi
Wakazi wa Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na mgomo wa manesi ambao umeanza hii Leo kote nchini wakisema kuwa mgomo huu unahatarisha maisha ya wananchi ambao wanategemea huduma za afya kutoka kwa hospitali za umaa.
Baadhi ya waliozungumza nasi wamesema kuwa mgomo wa manesi umetatiza utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit kwa sababu wengi wao ambao walikuwa wameraukia katika hospitali hiyo kupata matibabu wanarejea nyumbani bila kuhudumiwa.
Wamesema kuwa huenda pia huduma za akimama wajazito wanaokuja kujifungua katika hospitali ya serekali jimboni zikatatizika kwani wahudumu ambao wangefaa kuhakikisha kuwa huduma hizo imetolewa kwa njia inayofaa kwa sasa wapo kwenye mgomo.
Wameitaka idara ya afya pamoja na serekali ya kaunti ya Marsabit kuandaa kikao na viongozi wa manesi ili kuhakikisha kuwa wamepata suluhu kwani wanaoathirika ni wananchi ambao hawawezi kumudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi.