WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wahudumu wa afya kaunti ya Marsabit wameonywa dhidi ya kuendeleza dhuluma za kijinsia kama vile ukeketaji.
Wahudumu hao wa afya wametakiwa kulipa kipao swala la kulinda haki za binadamu na kuwasaidia katika kukomesha dhuluma za kijinsia.
Akizungungumza na idhaa hii baada ya zoezi la kuwapa hamasa wahudumu wa afya hapa mjini Marsabit, afisa wa jinsia katika shirika la kutetea hazi za kinadamu la MWADO Mary Nasibo amewaonya wahudumu hao wa afya kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria iwapo watapatikana wakiendeleza zoezi la ukeketaji.
Aidha, Nasibo amewatahadharisha wahudumu hao wa afya dhidi ya kuchukua hongo na kuzuia haki kutendeka katika kesi za dhulma za kijinsia.
Nasibo vilevile ametaja hoja ya hamasa kuzidi kutolewa kwa jamii ili kuhakikisha kwamba jimbo la Marsabit linapiga hatua katika vida dhidi ya dhulma za kijinsia.