KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya,
Town FC ndio mabingwa wa taji ya CRS youth Week baada ya kuilaza timu ya Sparks FC kwa jumla ya magoli mawaili kwa nunge katika fainali iliyogaragazwa katika uga wa shule ya upili ya Dakabaricha hapa mjini Marsabit.
Magoli ya Town FC yalitiwa kimyani na wachezaji Omar Wako kunako 27 na Lamar Mohamed kunako dakika ya 60.
Town FC ilifunzu fainali baada ya kuinyanyasa Chester FC kwa jumla ya magoli 4-1 katika awamu ya nusu fainali huku Sparks ikitinga fainaili baada ya kuitandika Jirime United kwa goli 1-0.
Town FC inabeba tuzo pamoja na shilingi 30,000 huku Sparks FC ikienda nyumbani na shilingi elfu 20,000.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani baada ya ushindi wa leo nahodha wa kikosi cha Town FC Walker Halche amesema kuwa watatumia fedha hizo kuweza kusajili wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi chao.