HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
.NA JohnBosco Nateleng
Kaunti ndogo ya Loiyangalani imeweza kutawala mashindano ya shule za msingi na JSS muhula huu kitengo cha kaunti baada ya kushinda voliboli pamoja na kandanda kwa mashindao hayo shule ya msingi na voliboli kwa shule ya msingi nganzi ya juu JSS.
Akizungumza na idhaa hii katika shule ya msingi ya Manyatta Jillo, mwenyekiti wa kaunti ndogo ya Loiyangalani na ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Ngoyoni, Ambrose Lepakio amesema kuwa mafanikio haya yametokana na mazoezi pamoja na ushirikiano uliopo baina ya wanafunzi na walimu toka Loiyangalani na kusema kuwa anatarajia ushirikiano huu uendelee hata katika kitengo cha mkoa(Regionals) ambayo inatarajiwa kusakatwa alhamisi wiki hii katika kaunti ya Meru.
Wakati huo huo, kocha wa voliboli kaunti ndogo ya Loiyangalani Wendi Dennis amesifia umoja uliopo baina yao na wanafunzi kuwa ndio chanzo kuu ya wao kutwaa ubingwa wa voliboli, kitengo cha shule ya msingi na msingi ya nganzi ya juu JSS mtawalia.
Kwa upande wake James Lokaru ambaye ni nahodha wa timu ya voliboli ameelezea kuwa wanajiaminia kuwa watawakilisha vyema kaunti ya Marsabit na pia kutarajia kufika kitengo cha taifa(Nationals).