HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
NA CAROLINE WAFORO
Serikali itaanza kufanya vikao vya ushirikishwaji wa umma kuhusu umuhimu wa vitambulisho vya kidijtali, maisha card.
Vikao hivyo vitakavyoanza mwezi huu wa Septemba vitaongozwa na machifu huku wakaazi jimboni Marsabit wakitakiwa kuhudhuria.
Haya yamewekwa wazi na naibu kamishna wa Marsabit ya kati Kefa Marube wakati wa kikao cha ushirikishwaji wa umma kuhusu sheria za usajili wa vyeti vya kuzaliwa, vya kifo pamoja na Maisha Card.
Kikao hicho kimewaleta pamoja washkau mbalimbali wakiwemo wakuu katika idara ya usalama, maafisa kutoka afisi ya usajili, machifu, wanaharakati pamoja na wasimamizi wa vijana katika sekta ya boda boda na ambao watasaidia katika vikao vinavyotarajiwa kuandaliwa.
Kefa anasema kuwa vitambulisho hivi vya kidigitali vina manufaa mengi kwani vinasaidia kuondoa ulaghai ulioko wakati wa kupata vitambulisho.
Naye afisa wa usajili jimboni Marsabit Michael Oduor amewatahadharisha wakaazi dhidi ya kulaghaiwa na watu wanaodai kutoka katika afisi ya usajili na kisha kuwalagha fedha. Amesema kuwa malipo yote yanafanywa kupitia mfumo wa E-Citizen.
I