KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya
Tuko tayari kurejea kazini na kuendeleza majukumu yetu ila lazima serekali ya kaunti itimize matakwa yetu kwanza.
Ndio kauli yake katibu wa muungano wa maafisa wa kliniki katika kaunti ya Marsabit Abdi Shukri.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Shukri ametaja kwamba maafisa wa kliniki wapo tayari kwa mazungumzo kati yao na serekali ya kaunti ya Marsabit ili kufikisha kikomo mgomo ambao umedumu kwa zaidi ya miezi 3 sasa tangu tarehe 17 mwezi aprili mwaka huu.
Shukri ametaja kwamba baadhi ya maswala ambayo wengehitaji serekali ya kaunti ya Marsabit kutimiza kabla ya wao kusitisha mgomo ni ikiwemo malipo ya mshahara wa mwezi Novemba mwaka jana sawa na mishahara ya wanafunzi wa nyajani maarufu Interns pamoja na kupandishwa vyeo kwa maafisa wa kiliniki haswa waliogeza viwango vya elimu.
Mengine ni ikiwemo bima ya afya kwa maafisa hao wa kliniki ambayo kulingana na Shukri imekuwa ikiwabagua baadhi yao.
Kadhalika Shukri ameweka wazi kuwa kuongezwa kwa idadi ya maafisa wa kliniki wanaohudumia wananchi wa Marsabit kama jambo wanalotaka pia litatuliwe ili kufanikisha huduma bora za afya kwa WanaMarsabit.