HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Caroline Waforo,
Mwanamke moja mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa na lita 23 za changaa katika eneo la mabatini Lokesheni ya Nagayo kaunti ya Marsabit.
Mwanamke huyo ambaye amekamatwa mara kadhaa na kuachiliwa hii ikiwa mara ya nne anaendelea kuzuiliwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani jumanne wiki ijayo.
Kulingana na OCS wa Marsabit Edward Mabonga kukamatwa kwa mama huyo ni kutokana na operesheni kali ya pombe haramu na mihadarati inayoendeshwa na maafisa wa usalama.
Haya yanajiri huku mwanaharakati wa kupigana na dawa za kulevya na mihadarati jimboni Marsabit Fredrick Ochieng akiwataka wazazi jimboni kujukumika katika malezi ya wanao ili kuwaepusha na utumizi wa dawa za kulevya.
Aidha Ochieng ametoa hamasisho kwa wakaazi jimboni kushirikiana na idara ya usalama katika kutoa taarifa muhimu ili kufanikisha vita dhidi ya pombe haramu na mihadarati.
Ochieng kadhalika amewatahadharisha vijana dhidi ya kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya ili kulinda maisha yao ya usoni.