IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Isaac Waihenya & Naima Abdulahi,
Onyo kali limetolewa kwa vijana wanaoendeleza wizi katika boma za watu hapa mjini Marsabit na vyunga vyake.
Akitoa onyo hilo chifu wa Marsabit mjini Hussein Charfi amewatahadharisha vijana waneoenedeleza kasumba hiyo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Chifu Charfi aliyezungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya Simu amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanajua majirani zao na pia kuwa wangalifu ili kuzuai visa vya wizi.
Kauli yake inajiri siku chache baada ya visa kadhaa vya uvujaji wa nyumba kuripotiwa katika maeneo ya Shauri Yako.
Aidha kuhusiana na swala la vijana waliochini ya umri wa miaka 18 kufanya biashara ya bodaboda hapa mjini Marsabit haswa kipindi hichi cha likizo,Chifu Charfi ametaja kwamba ofisi yake itafanya uchunguzi na kuchukua hatua hitaji kwa wale watakaopatikana na kosa hilo.