Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Isaac Waihenya & Farida Mohamed
Serekali ya kitaifa imejitolea kushughulikia maswala yanayowadhiri vijana hapa jimboni Marsabit.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi katika idara ya vijana kaunti ya Marsabit Joseph Maina.
Akizungumza baada ya kuandaa mkao na viongozi wa vijana katika eneo bunge la Saku,Maina amesema kuwa mkao huo umelenga kuwasikiliza vijana na pia kusaka suluhu kuhusiana na maswala ambayo yamekuwa yakiwaadhiri kwa muda.
Maina ameahidi kuwa serekali ya kitaifa itaboresha na kujenga upya kituo cha vijana (Youth Empowerment Center) katika kaunti ya Marsabit.
Aidha Maina amewarai vijana kukumbatia mikopo inayotolewa na serekali kwa vijana kama Uwezo Fund na Youth Fund ili kujiendeleza kimaisha.
Baadhi ya masuala ambayo yameibuliwa na vijana waliohudhuri wakiogozwa na muratibu wa maswala ya vijana Steve Roba na karani wa bunge la SYA Halima Abdikadir ni ikiwemo ongezeko la ulanguzi na uraibu wa dawa za kulevya ambapo wamemrai Maina kushirikiana na kamishina wa kaunti ya Marsabit ili kuhakikisha kwamba wanaoendeleza biashara hiyo wanachukuliwa hatua kali za kisheria.