Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Isaac Waihenya,
Serekali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya huduma za jamii inapania kuandaa mashindano ya riadha ya watu wanaoishi na ulemavu haswa wanaotumia magari ya magurudumu maarufu Wheel Chairs.
Kwa mujibu wa mkurugenzi katika idara ya huduma za jamii kaunti ya Marsbit Galgallo Okotu ni kuwa zoezi hilo linatajiwa kufanyika tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu huku watakaoshinda wakitarajiwa kuiwakilisha kaunti ya Marsabit kwa mashindano hayo viwango vya kaunti katika kaunti ya Isiolo kuanzi tarehe 11 hadi 12 mwezi uo huo wa Oktoba.
Akizungumza na Radio Jangwani ofisini mwake Galgallo ametaja kwamba zoezi hilo linalenga kuwapa watu wanaoishi na ulemavu hapa jimboni nafasi sawa ya kushiriki riadha kama watu wengine.
Kando na hilo Galgallo ametaja kwamba idara hiyo inalenga pia kuhakikisha kwamba wanawake wanaoishi na ulemavu kutoka hapa jimboni wanashiriki katika mashindano ya urembo yatakayoandaliwa jimboni Isiolo.
Aidha Galgallo ameirai jamii kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwahusisha katika miradi ya kijamii nay a maendeleo kama watu wengine.