HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Mashindano ya Muhula wa pili ya shule ya msingi na JSS kitengo cha kaunti yameng`oa nanga hii leo katika eneo bunge la Saku.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipee mwalimu Abdud anayesimamia michezo katika shule ya msingi ya Manyatta Jillo amesema kuwa shule zote zilizoweza kufuzu katika mashindano ambayo yaliyoandaliwa katika kaunti ndogo wamefika katika eneo la Saku tayari kushiriki mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kukamilika hapo Kesho Jumanne.
Abdub ameelezea kuwa timu ambayo itashinda siku ya Jumanne itawakilisha kaunti ya Marsabit Alhamisi katika mashindano ya Ukanda (Regionals) ambayo yatafanyika katika kaunti ya Meru.
Mwalimu Abdub ameelezea kuwa mashindano haya ni ya manufaa kwa wanafunzi hawa wa shule ya msingi kwani inawasaidia kutambua talanta zao na pia kuja pamoja kutoka maeneo tofauti jimboni inasaidia kukuza amani ya kudumu.