HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Caroline Waforo,
Magonjwa ya tumbo, gastritis, mafindofindo au tonsillitis pamoja na ugonjwa wa kisukari diabetes ni kati ya magonjwa yanaonekana kuwaathiri wengi wa wagonjwa katika kaunti ya marsabit.
Hii imebainika wakati wa utoaji wa huduma za bure za matibabu zilizotolewa na Membley Community Chapel kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Marsabit na AMREF baina ya Jumatatu iliyopita na hapo jana Jumatano.
Kulingana na afisa wa mawasiliano katika shirika hilo Prudence Komu takriban wagonjwa 1,100 waliweza kunufaika na huduma hizo.
Prudence anasema kuwa wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali walifika kutafuta huduma hizo ikiwemo kutoka eneobunge la northhorr.
Kulingana na prudence wagonjwa hawakutozwa chochote kupokea matibabu hayo ikiwemo dawa.
Aidha ameonyesha matumaini ya kurejelea huduma hizo mwaka ujao.