Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Isaac Waihenya,
Idara ya maji katika kaunti ya Marsabit imesaamba tenki za plastiki za maji za lita 5,000 kwa kaya 450 za hapa jimboni Marsabit.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo afisa mkuu katika idara ya maji Roba Galma, amesema kuwa zoezi hilo linalenga kupunguza changamoto za uhaba wa maji, hasa nyakati za ukame.
Galma ametaja kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit imejitolea kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safa na salama kwa matumizi yao ya kila siku.
Aidha amewataka wananchi kutunza tenki hizo huku akikariri kuwa idara hiyo imesambaza zaidi ya tenki 20,000 za maji kwa wanaMarsabit tangu mwaka wa 2017.
Baadhi ya wananchi walionufaika na tenki hizo wameishukuru serekali ya kaunti ya Marsabit kwa kile wamekitaja kwamba ni ‘kujali maslahi yao.’