HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Caroline Waforo,
Idara ya elimu katika kaunti ya Marsabit imependekeza kwa wizara ya elimu kuhamishwa kwa shule ya msingi ya El Molo bay iliyoko wadi ya Loiyangakani kaunti ya Marsabit kutokana na kufura kwa ziwa Turkana.
Haya ni kulingana na mkrugenzi wa elimu jimboni Marsabit Peter Magiri.
Magiri aliyezungumza na Shajara Ya Radio Jangwani afisini mwake amesema kuwa shule hiyo pamoja na shule ya msingi ya Layeni zinaendelea kuhatarisha maisha ya wanafunzi katika eneo hilo.
Aidha Magiri amesema kuwa ili zoezi hilo kufanikishwa itawalazimu wakaazi wanaoishi katika kisiwa cha Elmolo Bay kuhamishwa hadi katika eneo salama ambapo shule nyingine itajengwa.
Na huku mtihani wa KPSEA ikitarajiwa kuanza hivi karibuni Magiri anasema kuwa idara yake itahakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanakalia mtihani huo.
Ameahidi kuandaa mkutano maalum kesho Alhamisi utakao shirikisha washikadau mbalimbali katika idara ya elimu ili kujadili hatma ya wanafunzi hao.
Kuhusiana mikasa ya moto inayoendelea kushuhudiwa katika shule mbalimbali nchini Magiri amesema kwamba idara ya elimu hapa jimboni imeweka mikakati kuhakikisha kuwa visa sawia haviripotiwi jimboni.
Amesema kuwa hivi karibuni manaibu kamishana wataandaa mikutano ya kiusalama na wakuu wa shule ili kuweka mikakati zaidi.