WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Na Isaac Waihenya,
Vijana wa bunge la vijana wa Saku (SYA) wamelaani mauaji ya usiku wa kuamkia ana ambapo watu wanane waliuwawa katika eneo la Elle-Dimtu,Northhorr kaunti ya Marsabit.
Wakiongozwa na spika wa bunge la kaunti ya Marsabit Abdulaziz Boru vijana hao wametaja kwamba ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba watu wasio na hatia wanapoteza maisha yao mikononi mwa wahuni.
Vijana hao wameitaka idara ya usalama kuwachukulia hatua za kisheria waliotekela uovu huo ambao wanautaja kwamba unalenga kurejesha nyuma hatua za uiano zilizopigwa jimboni Marsabit.
Aidha Boru amewata vijana kutotumia mitandao ya kijamii kueneza chuki na badala yake kueneza jumbe za Amani na upendo.
Kwa upande mratibu wa maswala ya vijana katika bunge la vijana la Saku (SYA)Steve Roba amewarai vijana kutokubali kutumika kuzuia taharuki huku akimtaka kamishina wa kaunti ya Marsabit kuhakikisha kwamba jimbo la Marsabit linasheheni Amani ambayo imekuwa ikishuhudiwa.