HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
NA GRACE GUMATO
Ni afueni kwa shule ya bweni ya wasichana ya Loglog girls baada ya shirika lisilo la kiserikali la KDEF kujenge nyumba ya walimu iliyofunguliwa rasmi hii leo katika shule hiyo.
Akizungumza katika halfa hiyo Ahmed Kura ambaye ni mkurungezi wa KDEF ni kuwa Zaidi ya shule 100 katika eneo bunge la Laisamis zimeweza kujengewa nyumba ya walimu huku akitaja kuwa walimu ni watu muhimu katika jamii kutokana na jukumu lao la kupiga jeki swala la elimu.
Hata hivyo amesema kuwa changamoto ni kwa wazazi ambao hawadhamini masomo akiwashauri wazazi kupeleka watoto shule za karibu kutokana na gharama ya chini.
Aidha Ambrose Harugura ambaye ni mkurungenzi wa bodi ya kuajiri wafanyakazi wa kaunti amesema kuwa kwa miaka ya nyuma jamii za wafugaji zimekuwa nyuma sana kwa maswala ya elimu huku akishukuru shirika la KDEF kwa kuwasaidia jamii za wafugaji katika kupiga jeki swala la elimu.
Mwalimu mkuu wa shule ya Logologo Rose Sagaram amerudishia shirika la KDEF shukrani kwa kujengea nyumba walimu wake sawa na ofisi muhimu
Hata hivyo Alio Abdulahi ambaye ni mkurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo ya Laisamis amesema kupitia shirika hilo watoto wengi wameweza kurudi shule na kulipiwa karo hivyo amewahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule akitaja jamii za wafugaji kuwa na hulka ya kupeleka watoto wao kuchunga mifugo.