Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Caroline Waforo,
Afisa moja wa akiba NPR katika wadi ya Loiyangalani eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit amekamatwa kwa kumiliki bunduki tatu kinyume cha sheria.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa afisa huyo wa akiba kutoka kaunti ya Samburu alikamatwa katika barabara ya Ilaut wadi ya Loiyangalani alhmaisi ya tarehe 5 mwezi huu wa septemba.
Afisa huyo alikuwa kwenye piki piki pamoja na mwenzake aliyefanikiwa kutoroka.
Maafisa wa polisi walifanikiwa kupata bunduki tatu aina ya AK 47, FN, M16 rifle, magazine moja na risasi 3 zilizokuwa zimefichwa ndani ya gunia.
Mshukiwa amefikishwa katika mahakama ya Marsabit leo hii mbele ya hakimu Simon Arome ambapo ameachiliwa kwa bondi ya shilingi 1,000,000, kesi hiyo ikitarajiwa kusikilizwa tarehe 19 mwezi huu wa Septemba.
Mshukiwa alikamatwa wakati ambapo maafisa wa polisi walikuwa wakiendesha oparesheni ya kuwarejesha ngamia 17 walioibwa katika kijiji cha Sarima wadi ya Loiyangalani alhamisi wiki jana.
Alhamisi hiyo maafisa walifanikiwa kuwapata Ngamia 11 katika eneo la ruai kule mt kulal huku wengine 6 wakipatikana hiyo jana katika maeneo ya civicon wadi ya Loiyangalani na eneo la Nyiro Samburu kaskazini.
Kamanda Kimaiyo ametoa onyo kali kwa wzi wa mifugo akisem akuwa watakabilia vilivyo.