IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Wakaazi wa Hulahula Marsabit washabikia kisima kipya cha KDEF wakitaja kuwapunguzia safari ndefu ya kusaka maji.
Na JB Nateleng
Ni afueni kwa wakazi wa Hulahula, eneo bunge la Saku baada ya shirika lisilo la Kiserekali la Kenya Dryland Education Fund kuwekeza kwenye mradi wa kuwajengea kisima cha maji karibu na makazi yao.
Ni afueni kwa wakazi wa Hulahula, eneo bunge la Saku baada ya shirika lisilo la Kiserekali la Kenya Dryland Education Fund kuwekeza kwenye mradi wa kuwajengea kisima cha maji karibu na makazi yao.
Baadhi ya wakazi waliozungumza na idhaa hii wamesema kuwa hatua hiyo itawasaidia katika kuhakikisha kuwa wamepata maji kwa ukaribu hivyo kuwapunguzia masafa ambayo walikuwa wakitembea ili kuweza kuteka maji.
Wameelezea kuwa kisima hicho kitawasaidia wakazi wengi wa Hulahula kuweza kupanda miti na pia kulima mashamba kwa wingi hivyo kuwafanya waweze kujiboresha kiuchumi.
Kadhalika wakazi hao wamesema kuwa uwepo wa kisima hicho katikati mwa Kijiji cha Hulahula utaimarisha usalama wao kwani majambazi walikuwa wakiwavamia mara kwa mara wanapoelekea kuteka maji katika kisima kilichokuwa ndani ya msitu wa Marsabit.