KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Samuel Kosgei
IDARA ya utabiri wa hali ya hewa Marsabit imesema kiwango joto cha sentigredi zaidi ya 30 wakati wa mchana itashuhudiwa katika sehemu kadha za Marsabit ikiwemo kaunti ndogo za North Horr na Laisamis.
Kiwango joto nyakati za usiku haswa kaunti ndogo ya Saku inatarajiwa kushuka hadi sentigredi 15°c na sentigredi 18°c katika kaunti ndogo ya Moyale
Kwenye taarifa ya wiki mzima kuhusu hali ya hewa kaunti ya Marsabit, mkurungenzi wa idara hiyo Abdi Dokata amesema kuwa uwepo wa jua utashuhudiwa katika sehemu nyingi jimboni huku mawingu yakitarajiwa kutanda nyakati za usiku.
Dokata pia anasema baadhi ya sehemu kaunti ya Marsabit huenda ikashuhudia mvua za asubuhi. Sehemu hizo anasema ni pamoja na hapa Saku, Moyale, Dukana na hata Illeret iliyo kaunti ndogo ya North Horr.