Local Bulletins

Polisi wameanzisha msako dhidi ya majambazi waliovamia kituo cha polisi cha Lerata kaunti ya Samburu na kumuua afisa wa polisi.

Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac,

Polisi katika kaunti ya Samburu wameanzisha msako dhidi ya majambazi waliovamia kituo cha polisi cha Lerata karibu na kituo cha kibiashara cha Archers na kumuua afisa wa polisi mnamo siku ya jumapili.

Afisa huyo konstebo Moses Mwambia alipigwa risasi alipokuwa akichota maji.

Inaarifiwa kuwa genge hilo lilienda kituoni na kuomba maji ya kunywa na afisa huyo alipokwenda kwenye tanki lililokuwa karibu kuwachotea maji, alipigwa risasi kutoka nyuma na kufa papo hapo.

Majambazi hao walitoroka baada ya kutekeleza uhalifu huo na hadi kufikia sasa nia yao bado haijajulikana.

Kisa hichi kinajiri siku chache tu baada ya afisa mwingine wa polisi kuuwawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Pura kaunti ya Samburu mnamo usiku wa kuamkia sikuku ya Krisimasi katika shambulio lingine la kijambazi.

Wavamizi hao waliteketeza manyatta kadhaa na kuiba mifugo walioachwa na wanakijiji waliokuwa wametoroka eneo hilo kwa kuhofia usalama wao.

Wakti uo huo viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa Samburu Magharibi Neisula Olesuda wamekashifu matukio hayo na kuitaka idara ya usalama kuimarisha shughuli za upigaji doria.

Wamezitaka jamii za eneo hilo kuzungumza ili kutafuta suluhu la kudumu.

Subscribe to eNewsletter