Local Bulletins

Mawaziri Wapywa waapishwa na kuchukua majukumu yao rasmi katika ikulu ya rais

Na Machuki Dennson

Rais William Ruto amewaapisha mawaziri wake 22 hii leo katika ikulu yake ya Nairobi. Zoezi hilo limeongozwa na mkuu wa utumishi wa Umma Felix Kosgei mbele ya rais.

Rais amewaapisha mawaziri hao baada ya mkutano na wajumbe wa mrengo wa Kenya Kwanza katika ikulu hiyo.

Hiyo jana mawaziri hao waliidhinishwa na bunge la kitaifa na muda mfupi baadaye rais akawatangaza rasmi kuwa mawaziri kupitia gazeti rasmi la serikali.

Mawaziri wapya sasa ni kama ifuatavyo:

  1. Kiongozi wa mawaziri – Musalia Mudavadi
  2. mwanasheria mkuu – Justin Muturi
  3. waziri wa maswala ya ndani- Prof Abraham Kindiki
  4. waziri wa fedha na mipangilio ya kiuchumi – Prof. Njuguna Ndung’u
  5. waziri wa huduma za kitaifa na maswala ya jinsia – Aisha Jumwa
  6. waziri wa ulinzi – Aden Duale
  7. Waziri wa maji na usafi – Alice Wahome
  8. waziri wa maswala ya kigeni – Alfred Mutua
  9. waziri wa biashara, uwekezaji na viwanda – Moses Kuria
  10. waziri wa maswala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, maeneo kame na maendeleo ya ukanda – Rebecca Miano
  11. waziri wa barabara, uchukuzi na miundomsingi – Kipchumba Murkomen
  12. waziri wa mazingira na misitu – Soipan Tuya
  13. waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya miji – Zachariah Mwangi Njeru
  14. waziri wa utalii, wanyamapori na turathi za kitaifa – Peninah Malonza
  15. waziri wa kilimo na ufugaji – Mithika Linturi
  16. waziri wa afya – Susan Nakumicha Wafula
  17. waziri wa mawasiliano, habari na uchumi wa kidijitali – Eliud Owalo
  18. waziri wa elimu- Ezekiel Machogu
  19. waziri wa kawi na petroli – Davis Chirchir
  20. waziri wa michezo, Sanaa na maswala ya vijana – Ababu Namwamba
  21. waziri wa mashirika na biashara ndogo ndogo – Simon Chelugui
  22. waziri wa madini, uchumi wa maziwa kuu na bahari – Salim Mvurya
  23. waziri wa leba – Florence Bore
  24. Katibu wa baraza la mawaziri – Mercy Wanjau

Mawaziri hawa watachukua hatamu za uongozi kutoka mawaziri waliohudumu kipindi cha rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Subscribe to eNewsletter