Local Bulletins

Wawakilishi Wadi Kutoka Kaunti Ya Kisumu,Homabay Na Kaunti Ya Migori Wameahidi Kupitisha Mswada Wa Marekebisho Ya Katiba BBI.

Kinara Wa ODM Raila Ondiga Alipokutan Na Wajumbe Kutoka eneo la Nyanza.
Picha; Hisani

By Waihenya Isaac,

Wawakilishi wadi Kutoka kaunti ya Kisumu,Homabay na kaunti ya Migori wameahidi kupitisha mswada wa marekebisho ya Katiba BBI.

Kwenye Mkutano ulioandaliwa Katika kaunti Ya Kisumu wajumbe hao walitaja kuwa watafuata mfano wa bunge la kaunti ya Siaya kwa kupitisha mswaada huo kabla ya wiki hii kukamilika.

Akizungumza Katika Mkutano huo Kinara wa ODM raila Odinga amewataka wakenya kukumbatia Ripoti ya BBI huku akiitaja kama itakayoleta usawa kwa wakenya wa tabaka zote.

Raila ametaja kuwa eneo la Nyanza ni mojawepo ya maeneo yatakayofaidika na mageuzi ya Katiba huku akitaja kuwa rasilimali nyingi zitaelekezwa mashinani.

Kinara Wa ODM Raila Ondiga Alipokutana Na Wajumbe Kutoka eneo la Nyanza.
Picha; Hisani

Amewataka wananchi kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kikabila huku akiweka wazi kuwa eneo la Nyanza liko tayari kufanya kazi na viongozi wengine wa kisiasa ili kupeleka maendeleo.

Raila aidha amemchangamoto naibu rais William Ruto kujitokeza na kutangaza msimamo kuhusu BBI.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter