Local Bulletins

Wanaopinga Kura Ya Maoni Ya BBI Wanapaswa Kutumwa Nyumbani Kwa Kutochaguliwa Katika Uchaguzi Mkuu Wa 2022.

Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

Mwakilishi wa Mwanamke wa Homa Bay Gladys Wanga sasa anasema wanasiasa wote wanaopinga kura ya maoni ya BBI wanapaswa kutumwa nyumbani kwa kutochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Wanga amesema haitakuwa haki kwa wanasiasa hao kuruhusiwa kutekeleza BBI ikiwa itapita ikizingatiwa kuwa hawana nia njema.

Mbunge huyo amesema sababu kuu ya Katiba ya 2010 kutotekelezwa vyemani kufikia sasa, ni kwa sababu ilitua mikononi mwa wale ambao waliipinga katiba hiyo.

Wanga anasema kuwa yeyote anayepania kuchaguliwa mwaka ujao anafaa kuunga mkono mswada wa BBI kwani inalenga kuunganisha nchi.

Matamshi yake Wanga, yameungwa mkono na kamishna wa tume ya kitaifa ya jinsia na usawa –NGEC, Priscilla Nyokabi anayesema kuwa wanasiasa wakuu watatu nchini wanafaa kuweka juhudi zao ktk suala la BBI.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter