Local Bulletins

Wakenya Waingia Mwaka 2021 Wakiwa Na Matumaini Ya Mwaka Bora Zaidi Ya Mwaka Jana

Picha; Hisani

By Machuki Denson

Wakenya Wengi Wana Matumaini Kwamba Mwaka Wa 2021 Utakuwa Wa Mafanikio Kuliko Wa 2020 Kulingana Na Utafiti Wa Kura Ya Maoni.

Utafiti Huo Uliofanywa Na Kampuni Ya   Infotrak,  Ambao Mtokeo Yake Yalitolewa Leo Unaonyesha Kwamba Asilimia 61 Ya Wakenya Wana Matumaini Makubwa Kwamba  2021 Utakuwa Mwaka Mzuri  Ukilinganishwa Na Mwaka Unaokamilika.

Wengi Wa Waliohojiwa – Asilimia 95 Wamesema 2020 Ulikuwa Mwaka Mgumu Sana Katika Maisha Yao.

Utafiti Huo Ulifanywa Kati Ya Disemba Tarehe 27 Na Tarehe 29  Na Uliwahusisha Watu 800.

Wakenya Wengi Walitaja Ukosefu Wa Ajira , Gharama Ya Juu Ya Maisha Na Ugumu Wa Kupata Huduma Za Afya Kama Mambo Yanayowatatiza.

Asilimia 44 Ya Waliosema 2020 Ulikuwa Mwaka Mgumu Walitaja Ukosefu Wa Fedha  Kama Sababu Kuu Ilhali Asilimia 24  Walipoteza Kazi Zao.

Asilimia 21  Walishuhudia Biashara Zao Zikiporomoka  Na Kuzifunga Ilhali Asilimia 2 Waliwapoteza Rafiki Au Jamaa Wa Karibu.

Eneo La Pwani Linaongoza Kwa Idadi Ya Watu Wengi Waliotaja Mwaka Wa 2020 Ama Mgumu  Kwa Asilimia 72   Likifuatwa Na Nyanza Kwa Asilimia 64.

Asilimia 62 Ya Wakaazi Wa Nairobi Waliutaja Mwaka Wa 2020 Kama Mgumu Zaidi Katika Maisha Yao  Ilhali Asilimia 61 Ya Wakaazi Wa Magharibi Waliripoti Kukumbana Na Ugumu Mwaka Wa 2020 .

Hali Haikuwa Na Makali Sana Katika Maeneo Ya Kaskazini Mashariki Kwa Asilimia 60, Rify Valley Kwa Asilimia 59 Na Eneo La Kati Kwa Asilimia 54.

Subscribe to eNewsletter