Local Bulletins

Wabunge Wanaounga Mkono Mwafaka Kati Ya Rais Uhuru Kenyatta Na Raila Odinga Kupanga Kumgatua Mamlakani Naibu Wa Rais William Ruto.

Naibu Wa Rais William Ruto Pamoja Na Aliyekuwa Gavana Wa Bomet Isaac Rutto Wakti wa Ziara Huko Bomet.
Picha; Hisani

By Waihenya Isaac,

Wabunge amabao wanaunga mkono mwafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga sasa wanapanga kikao cha pamoja na huenda wakaafikiana Kuhusu kumgatua mamlakani Naibu wa Rais William Ruto.

Kwa mujibu wa Mbunge  wa Kieni Kanini Kenga ni kuwa wabunge hao huenda wakawasilisha mswaada wa kutokuwa na Imani na Naibu wa Rais William Ruto kwa kile wanachokitaja kuwa kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na mbele ya umaa.

Kanini amesema kuwa Ruto alipanga kikao na wabunge ambao wanamunga Mkono na hivyo wanaomunga Mkono Rais pia hawatasita kupanga kikao.

Hiyo jana Kiongozi wa wengi Katika bunge la kitaifa Amos Kimunya Alisema kufikia sasa hana habari ya kuwepo mpango wa kuwasilisha hoja ya kutokuwepo na naimani na Naibu wa rais William Ruto na kusisitiza kwamba licha ya tofauti zilizopo atafanya kila jitihada kuhakikisha idara hiyo inatekeleza wajibu wake.

Kimunya alisema kuwa baada ya kurejelea vikao,wabunge wataipa kipau mbele  miswaada iliyokwama Katika kikao cha mwaka jana na pia mchakato wote wa BBI.

Siku za hivi maajuzi Chama Cha ANC kupitia mbunge wa Lugari Ayub Savula,kimetaja mara kadhaa kutaka kuwasilisha mswaada wa kutokuwa na Imani na Naibu wa Rais Bungeni.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter