Local Bulletins

Wabunge kurejea bungeni wiki ijayo tarehe 29 mara tu baada ya Krisimasi

majengo ya bunge ndani

Na Silvio Nangori

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi ameitisha kikao maalumu bungeni December tarehe 29, 2021 kuhusiana na mswada wa vyama vya kisiasa.

Katika notisi ya hapo jana Muturi amewataka wabunge wote kuhudhuria vikao vyote vya bunge kama ilivyotajwa na Kiongozi wa wengi Bungeni Dr. Amos Kimunya.

Kikao hicho kitafanyika mwendo wa asubuhi saa nne na kisha adhuhuri saa sita u nusu.

Maswala watakayozungumzia wabunge ni kama vile taarifa ya Rais Uhuru Kenyatta na vile vile kuwasilishwa kwa ripoti kutoka kwa kamati ya idara ya haki na maswala ya sheria katika mabadiliko ya mswada uliowasilishwa.

Aidha kutakuwepo kusomwa kwa mara ya tatu kwa mswada ya vyama vya kisiasa na vile vile mswada wa ununuzi wa Umma na utupwaji wa mali ikiwa miongoni mwa ajenda kuu.

Spika Muturi amewaamuru wabunge waliopendekeza mabadiliko katika mswada wa vyama vya kisiasa kujitokeza wenyewe December 28, 2021, ili kuangaliwa swala hilo kwa kina kabla ya kikao.

Siku ya Jumatano wiki hii naibu spika wa bunge la kitaifa Moses Cheboi alifutilia mbali mswada wa mabadiliko katika vyama va kisiasa baada ya wabunge kuzua purukushani.

 

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter