Local Bulletins

Vyama Vya ODM, KANU, NARC Na PNU Katika Kaunti Ya Isiolo Kufanya Kazi Kwa Umoja Ili Kuhakikisha Ripoti Ya BBI Inapata Uungwaji Mkono.

Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

Vyama vinne katika kaunti ya Isiolo kikiongozwa na chama cha ODM, KANU, NARC na PNU wamejitokeza na kudokeza kwamba watafanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha ripoti ya BBI inapata uungwaji mkono kutoka kwa wakaazi wa kaunti ya Isiolo.

Wakiongea na vyombo vya habari katika afisi za ODM mjini Isiolo, viongozi hao na wanachama wa vyama vinne wamedai kuwa lengo la BBI ni kuwauganisha wakenya wote bila kuzigatia misingi ya kikabila.

Hata hivyo viongozi hao wametoa wito kwa kamati ya kutekeleza BBI kutoa nakala za BBI kwa vyama ili wananchi waweze kupata nakala hizo. Viongozi hao wametupitilia mbali madai kuwa wakaazi wa isiolo wanapinga ripoti ya BBI.  wakati uo huo wameonekana kushabikia salamu kati ya Rais Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter