Local Bulletins

Sitachelea Kuanzisha Mswada Wa Kumtimua William Ruto Kutoka Chama Cha Jubilee – Asema Joshua Kutuny

Picha;Hisani.

By Samuel Kosgei,

Naibu katibu mkuu mpya wa chama cha Jubilee Joshua Kutuny amesema kuwa hawezi akachelea kuanzisha mswada wa kumtimua naibu wa rais William Ruto kutoka chama hicho tawala cha jubilee.

Hata hivyo Kutuny ambaye ni mbunge wa Cherangany amesema licha ya kuwa hajapokea taarifa zozote za kutimuliwa kwa naibu wa rais ataunga mkono mswada huo wa kutimuliwa kwake kwa ajili ya kumkosea nidhamu rais.

Kutuny ameteuliwa juzi kuwa naibu katibu wa jubilee akichukuwa nafasi yake Caleb Kositany  ambaye ni mwandani wa naibu wa rais William Ruto. Hatua hiyo ilionekana kama kumkata mikono naibu wa rais ambaye anatajwa kama anayemkaidi rais.

Kutuny amekuwa mkosoaji mkuu wa naibu wa rais William  Ruto ila alibadilisha mkondo huo 2013 alipoteuliwa  kuwa mshauri wa kisiasa wa rais Uhuru Kenyatta.

Wiki jana naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe alikuwa ameonya kutimuliwa kwa mbunge Kositany huku pia akidai naibu wa rais atafuata hivi karibuni.

Subscribe to eNewsletter