Local Bulletins

Sherehe za Krisimasi zanoga nazo ajali barabarani zikichacha

Fikiria usalama Barabarani, kaa salama, NTSA

Na Irene Wamunda

Watu wanne wameaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani ambayo imetokea katika eneo la Kerita Kaunti ya Uasin Gishu kwenye barabara kuu ya Eldoret kuelekea Nakuru.

Wanne hao wamefariki papo hapo baada ya gari lao walilokuwa wakiendesha kugongana ana kwa ana na gari jingine asubuhi ya Ijumaa, Disemba 24.

Gari hilo dogo linadaiwa kuendeshwa bila umakinifu kabla ya kugongana ana kwa ana na lori hilo lililokuwa likielekea Nakuru.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Uasin Gishu Ayub Gitonga amesema kuwa miili ya wahasiriwa imepelekwa katika makafani ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi mjini Eldoret

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter