Local Bulletins

Serekali Ya Kaunti Ya Wajir Imeanza Kutoa Chanjo Ya Ugojwa Wa Korona.

Picha:Hisani

By Waihenya Isaac

Serekali ya kaunti ya Wajir imeanza kutoa chanjo ya ugojwa wa  korona hii leo kwa wahudumu wa wafya Katika hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakti wa Uzinduzi wa zoezi hilo, Afisa mkuu wa afya Katika kaunti hiyo Adan Eno amesema kuwa  wahudumu wa afya, maafisa wa usalama  pamoja na waalimu ndio watakaopewa kipau mbele.

Aidha mkurungezi wa afya Daktari Dahir Snow amesema kuwa awamu ya kwanza ya kutoa chanjo itaendelea kwa kipindi cha miezi miwili na kisha awamu ya pili itawalenga wale wenye zaidi ya umri wa miaka 50 mbali na wanaougua saratani.

Kamanda wa polisi Katika kaunti hiyo Stephen Ngetich neye amawataka wananchi kupuuza uvumi unaoenelezwa kuhusiana na chanjo hiyo huku akitaja kuwa iko salama kwao.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter