Local Bulletins

Rais Uhuru Kenyatta Atakiwa Kutatua Mzozo Kati Ya TSC Na KNUT

Picha; Hisani

By Samuel Kosgei,

Mashirika ya Kimataifa ya kushughulikia matakwa ya walimu sasa yanataka mzozo wa muda baina ya Tume ya Huduma za Walimu,TSC na Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT kutatuliwa kwa haraka na Rais Uhuru Kenyatta

Mashirika hayo mawili, Education International na International Trade Union Confederation,  yameitaka TSC kukoma kuwaondoa walimu wa KNUT katika sajili yake.

Aidha yanamtaka rais Kenyatta kuongoza mazungumzo baina ya TSC na Knut ili kumaliza mzozo ambao unazidi kuathiri pakubwa shughuli za elimu kupitia malumbano ya kila mara.

Kupitia barua kwa rais, mashirika hayo yatanaka TSC kukomesha vita dhidi ya KNUT na kulegeza masharti makali ambayo yamewekewa wanachama wa KNUT.

Wakuu wa masharika hayo, Dakta Christian Addai -Poku na Dennis Sinyolo wamesema wakati umefika kwa TSC kuacha kuwatenga walimu wa KNUT katika kuwapandishwa vyeo na kuwaongeza mishahara walimu.

Ombi hilo linajiri wakati, KNUT wiki iliyopita ikielekea mahakamani kuishtaki TSC kwa kukiuka maagizo ya mahakama kuhusu mzozo baina yao

Subscribe to eNewsletter