Local Bulletins

Rais Kenyatta Awapongeza Wakilishi Wadi Mbali Mbali Nchini Waliopitisha Mswaada Wa Maridhiano BBI.

Rais Kenyatta Alipokuwa Akiwahutubia Wananchi katika eneo la Kayole jijini Nairobi.
Picha;Hisani

By Silivio Nangori,

Rais Uhuru Kenyatta amewapongeza wakilishi wadi mbali mbali Nchini waliopitisha mswaada wa maridhiano BBI.

Akizungumza katika eneo la kayole jijini Nairobi katika Hafla ya Kufuangua Hospitali,Rais amesema kwamba serikali yake itaendelea kushughulikia maendeleo ya nchi.

Aidha Kenyatta amewataka viongozi  kuungana kutatua matatizo kwa sauti moja kuliko kuleta vurugu na tofauti miongoni mwa wananchi.

Amewataka viongozi wasitumie vyeo vyao kuwakandamiza na kuchochea watu kwa ajili ya ukabila kwa kila mkenya ana haki ya kuishi katika nchi ya Kenya.

Kuuhusiana na kuungana kwake na kinara wa ODM Raila Odinga, Rais Kenyatta amedai kuwa kumeleta Amani Nchini.

Aidha amewataka wananchi wote kuunga Mkono mswaada wa  maridhiano  BBI akidai kwamba una  manufaa chungu nzima kwa mkenya wa kawaida.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter