Local Bulletins

Polisi wachunguza kisa cha utekajinyara kwa Dennis Itumbi

Dennis Itumbi akihudumiwa hospitalini jana usiku.

Na Silvio Nangori

Idara ya polisi imewataka wakenya kukoma kuenbdeza uvumi usio na msingi kuhusiana na madai ya utekajinya kwa mwanablogi na mshirika wa karibu wa naibu rais William Ruto Dennis Itumbi.

Itumbi ambaye amepatikana jana usiku akiwa hai anadaiwa kutekwa nyara jana Alhamisi alipokuwa akitoka kwenye kinyozi.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa polisi Bruno Shioso ni kwamba tayari wamenzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Amewarai wananchi walio na taarifa yoyote kuhusiana na kutekwa nyara kwa Mwanablogi Dennis Itumbi kuwasiliana na idara ya polisi.

Shioso amesema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Thindigua kaunti ya Kimabu.

Ripoti kwenye mitandao ya kijamii zilifichua kuwa Itumbi alitekwa nyara na kuwekwa ndani ya gari ambalo lilitoweka bila kujulikana.

 

Idara ya polisi hata hivyo imekanusha kuwa mwanablogu huyo alikuwa chini ya ulinzi wake.

Kulingana na Seneta wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen, Itumbi alipatikana akiwa uchi wa mnyama na akiwa amepigwa kikatili na kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.

 

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter