Local Bulletins

NCPB Kuongeza Bei Ya Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima

Picha;Hisani

By Adano Sharawe,

Bodi Ya Kitaifa Ya Nafaka Na Mazao (NCPB) Itaongeza Bei Ya Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima Baada Ya Idadi Ndogo Ya Wakulima Kujitokeza Kuuza Mazao Yao Katika Maghala Ya Eldoret.

Wakulima Wakiongozwa Na Mkurugenzi Wa Shirika La Wakulima Kaskazini Mwa Bonde La Ufa Kipkorir Menjo Wamesema Kuwa Idadi Hiyo Ndogo Imesababishwa Na Bei Duni Ambayo Serikali Imetangaza Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima.

Wakizungumza Na Wanahabari Mjini Eldoret, Wakulima Hao Wameishinikiza Serikali Kuongeza Bei Ya Zao Hilo Ili Kuwaondolea Wakulima Hasara.

NCPB Imefanikiwa Kununua Magunia 2000 Pekee Ya Mahindi Tangu Ilipoanza Kununua Kutoka Kwa Wakulima Wakati Wa Kuanza Kwa Msimu Wa Sherehe Ya Krismasi Mwaka Uliopita.

Wakulima Wanasusia Bei Ya Sh2,500 Inayotolewa Na NCPB Kwa Gunia La Kilo 90.

Kwa Upande Mwingine, Wafanyabiashara Hununua Gunia La Mahindi La Kilo 90 Kwa Sh2,700, Hivyo Kuwa Vigumu Kwa NCPB Kuvutia Mazao Kutoka Kwa Wakulima.

NCPB Ilifungua Milango Yake Kwa Wakulima Mwaka Jana Baada Ya Kushindwa Kununua Mahindi Kutoka Kwao 2019.

 

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter