Local Bulletins

Mzee Mmoja Amuua Kwa Kumkatakata Mwanawe Mwenye Umri Wa Miaka 43 Kijiji Cha Karugu Kilichoko Eneo La Gikuu Embu Mashariki Kaunti Ya Embu.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Hali ya huzuni imekikumba kijiji cha Karugu kilichoko eneo la Gikuu Embu mashariki kaunti ya Embu baada ya mzee mmoja kumuua kwa kumkatakata mwanawe mwenye umri wa miaka 43.

Inadaiwa kuwa maremu Alexender Munene aliyekuwa mlevi alikuwa ameenda kutatua mzozo baaina ya wazazi wake,wakati babake mzazi Benjamin Njiri Bendan alipomgeukia akitumia panga kwa kumshambulia na kumkatakata hadi akaaga.

Wakaazi wa eneo hilo walisema kuwa waliskia mayoe na vurungu katika boma la mzee huyo lakini wakashangaa kuupata mwili wa marehemu Munene ukiwa umelowa damu na panga ikiwa kandokando ya mwili huo.

Mshukiwa alilazimika kuelekea katika kituo cha polisi cha Runjenjes baada ya wakaazi waliojawa na ghadhabu kutishia kumuua.

Kwa sasa mshukukiwa huyu anazuiliwa Katika kituo cha polisi cha Runyenje huku mwili wa mwanawe ukihifadhiwa katika  hospitali ya Runyenjes Level 4.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter