Local Bulletins

Mwanamume Mwenye Umri Wa Miaka 48 Amemuua Mkewe Akitumia Mshale Huko Elburgon Nakuru.

Picha;Hisani

By Jillo Dida Jillo,

Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 amemuua mkewe akitumia  mshale katika Kijiji cha Kaptimon huko Elburgon kaunti ya Nakuru kutokana na mzozo wa mahindi.

Kulingana na ripoti ya idara ya ujasusi ni kuwa, Wilson Koech mumewe marehemu alijaribu kuuza mahindi japo alipingwa na mkwewe na mwanawe.

Hata hivyo ripoti ya polisi imesema kuwa Koech alimkimbiza mwanawe Collins Kipchumba akitumia panga japo alinusurika.

Baada kwa hasira alimgeukia mwekewe mwenye umri wa miaka 43 na kumwangamiza kwa mishale hapo hapo.

Koech amekamatwa muda mfupi baadaye huku akisubiri kufikishwa mahakamani.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter