Local Bulletins

Mahakama Ya Runyejes Imefungwa Kuanzia Leo Baada Ya Wafanyakazi Wake 18 Kupatikana Kuugua Virusi Vya Corona.

Picha;Hisani

Na Adano Sharawe,

Mahakama ya Runyejes imefungwa kuanzia leo baada ya wafanyakazi wake 18 kupatikana kuugua virusi vya corona.

Kwenye taarifa, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu amesema kuwa uamuzi huo umefuatia mapendekezo ya maafisa wa wizara ya afya na kamati ya watumiaji mahakama katika mahakama hiyo ya Runyenjes kufuatia kuthibitishwa kwa visa vya maambukizi ya Corona miongoni mwa wafanyikazi.

Amesema kuwa mahakama hiyo itafungwa kwa siku 8 na kwamba maswala yote ya dharura yatahamishiwa mahakama ya Embu na Kerugoya.

Akiwatakia nafuu ya haraka wale walioathirika, kaimu jaji mkuu huyo alisema kuwa ili kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo, maafisa wa idara ya mahakama watajitenga kwa muda wa siku kumi.

Alisema kuwa mahakama hiyo itarejelea shughuli za kawaida mara tu hali itakapoimarika.

Haya yanajiri kutokana na wasi wasi kufwatia ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi ya corona nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter