Local Bulletins

Kaunti Zilizopo Mipakana Mwa Nchini Zimetakiwa Kuchukua Tahadhari Ili Kuzuia Wimbi Jipwa La Virusi Vya Korona.

Picha;Hisani

By  Waihenya Isaac,

Kaunti zilizopo mipakana mwa nchini zimetakiwa kuchukua tahadhari ili kuzuia wimbi jipwa la virusi vya korona.

Akizungumza alipozuru hospitali ya Rufaa ya Narok kaunti ya Narok hii leo waziri wa afya Mutahi Kagwe ametaja kuwa kaunti zilizopo Katika mipaka ya kenya na mataifa mengine zipo Katika hatari ya kupata wimbi hilo jipya la korona kutoka katika mataifa jirani.

Waziri Kagwe ametaja kuwa kaunti hizo zinafaa kutitilia mkazo swala la kuwapima watu wote wanaoingia hapa Nchini kupitia mipakani.

Huku Hayo Yakijiri.

Watu 174 wamepatikana na virusi vya Korona baada ya sampuli 2,848 kupimwa kwa muda was aa 24 zilizopita na kufikisha visa hivyo kuwa 103,188 huku umla ya sampuli zilizopimwa  kufikia sasa ni 1,246,279.

Katika visa hivyo vipya 174, 159 ni wakenya huku 15 wakiwa ni ni raia wa kigeni, wanaume wakiwa 92 ilhali wanawake ni 82.

Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja huku yule wa umri wa juu akiwa na umri wa miaka 79.

Aidha hii Leo watu 86 wamepona ugonjwa wa korona na kufikisha idadi ya watu waliopona virusi Hivyo kuwa 85,336.

Hata hiyo Watu wengine 2 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya ya watu waliofariki kutokana na janga hilo kuwa 1,797.

Wagonjwa 258 wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali nchini huku 1,190 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani.

 

Subscribe to eNewsletter