Local Bulletins

Kaunti tatu pekee kati ya 47 zilifanikiwa kuafikia shabaha ya ukusanyaji mapato katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21.

Mkaguzi wa bajeti Margaret Nyakang’o.
Picha; Hisani

By Adano Sharawe,

Kaunti tatu pekee kati ya 47 zilifanikiwa kuafikia shabaha ya ukusanyaji mapato katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21.

Ripoti ya mkaguzi wa bajeti Margaret Nyakang’o inaonyesha kuwa kaunti ya  Kirinyaga imeafikia makadirio yake katika miezi mitatu ya kwanza baada ya kukusanya jumla ya Sh92 milioni.

Migori ilikusanya Sh60.3 milioni huku Tana River ikifunga tatu bora baada ya kukusanya Sh19 milioni.

Katika kipindi hicho hicho, mapato ya jumla ya serikali za kaunti 47 yalididimia kutoka Sh7.7 bilioni hadi Sh5.9 bilioni.

Kwa mujibu wa Dk Nyakang’o, hii ni asilimia 11 ya shabaha ya kila mwaka ya Sh53 bilioni kupokelewa kutoka kwa vyanzo vya ndani.

Katika miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2020, kaunti 15 tu kati ya 47 ziliweza kukusanya zaidi ya Sh100 milioni kupitia mapato ya ndani.

Nairobi iliongoza orodha kwa Sh1.5 bilioni lakini ilishindwa kufikia shabaha yake.

Ikafuatiwa na Kiambu (Sh452.3 milioni), Nakuru (Sh294.2 milioni), Machakos (Sh206 milioni), Kakamega (Sh198.2 milioni) na Narok (Sh168.2 milioni).

Wakati huo huo, kaunti 17 zilisajili mapato ya chini ya Sh50 milioni.

Kaunti hizo ni Kisii (Sh41 milioni), Mandera (Sh38.1 milioni), Vihiga (Sh36.5 milioni), Kwale (Sh33.8 milioni), Marsabit (Sh26 milioni), Garissa (Sh25.8 milioni), West Pokot (Sh21 .7 milioni) na Bomet (Sh20.3 milioni).

Isiolo, Samburu na Nandi zinaburuta mkia kwa kuandikisha mapato ya Sh9.9 milioni, Sh8.2 milioni na Sh4.6 milioni mtawaliwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter