Local Bulletins

Kampeni Za Kupigia Debe Ripoti Ya BBI Kuanza Jumatatu Wiki Ijayo.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Kamati ya kitaifa ya mpango wa BBI imetaja kuwa itanza kampeni za kupigia debe Ripoti hiyo kuanzia jumatatu wiki ijayo.

Kwa mujibu wa viongozi wa kamati hiyo,Junet Mohamed na Denis Waweru ni kuwa mipango ya kuanza kampeni za kuipa umaarufu zaidi ripoti ya BBI imekamilika.

Viongozi hao walikuwa wameandaa kikao cha  pamoja na wabunge tofauti walioyapongeza mabunge ya kaunti kwa kupitisha mswaada huo na kuuelekeza katika hatua nyingine.

Aidha wameitaka idara ya Mahakama  kuharakisha kesi zilizowasiliswa mahakamani kupinga mswada huo ili isiadhiri mipango ya kura ya maoni.

Kadhalika Wabunge waliohudhuria kikao hicho wameahidi pia kuupisha mswaada huo bungeni.

Kufikia sasa mabunge 41 ya kaunti yamepitisha mswada huo, huku Bunge la Kaunti ya Baringo likiwa la kipekee lililoukataa.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter