Local Bulletins

Hazina ya afya ya kitaifa NHIF yadai serekali ya kaunti ya Marsabit deni la shillingi milioni 36.

Picha:Hisani

Na Samuel Kosgei,

Mwakilishi wadi wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot amedai kuwa ahadi ya gavana wa Marsabit kulipia baadhi ya watu maskini bima ya afya kupitia bima ya NHIF huenda isitimie kutokana na deni la Zaidi ya shilingi milioni 36 ambalo serikali ya kaunti inadaiwa na hazina ya kitaifa afya NHIF.

Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Tomasot anadai kuwa wao kama wawakilishi wadi tayari walitenga pesa zitakazofanikisha mradi huo hivyo wanashangaa mbona utekelezwaji wake haupo kufikia leo.

Mradi huo awali kulingana naye ulilenga familia 10, 000 kote jimboni ili waweze kulipiwa pesa hizo za bima ya afya.

Wakti uo huo amedai kuwa wao kama Mcas wamekuwa wakitenga shilingi milioni 60 kila mwaka wa kifedha ili ifanikishe mradi huo ila kufikia leo anasema kuwa bado wananchi wanakosa kupokea huduma afya bila malipo.

Subscribe to eNewsletter